Ijumaa, 25 Oktoba 2013

BISHOP SPEAR MWAIPOPO:

BISHOP SPEAR MWAIPOPO:

Ubatizo wa Roho Mtakatifu:

Ubatizo wa Roho Mtakatifu:
Waamini wote wanatakiwa na wanayo haki ya
kutafuta ahadi ya baba, yaani ubatizo wa Roho Mt
na moto, kulingana na     agizo la Bwana wetu Yesu Kristo.
Huu ulikuwa ni ujuzi wa kawaida kwa wote
waliokuwemo katika kanisa la mwanzo la Kikristo.
Pamoja na huo ubatizo huja uwezo kutoka kule juu kwa ajili
ya maisha ya utumishi, na kutolewa kwa karama     pamoja na
matumizi yake katika     huduma (Lk.24.24:49; Mdo.1:4;8; 1Kor.12:1-31).
Ujuzi huu ni tofauti kabisa     ingawa unalingana na ujuzi wa kuzaliwa upya
(Mdo.812-17, 10:44-46; 11:14-16; 15:7-9). Pamoja na ujuzi huo wa ubatizo
katika Roho Mtakatifu kunakuja ujuzi mwingine kama kujazwa mpaka kufurika kwa Roho Mt
(Mdo.2:43, Ebr.12:28), kujitoa kwa hali ya juu kwa ajili ya Mungu na kujiweka wakfu kwa
ajili ya kazi yake (Mdo.2:42), pamoja na upendo wenye vitendo     zaidi kwa Kristo na kwa
Neno lake na kwa wanaopotea (Mk. 16:20).